Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa

Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa

Katika ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa, mfupa wa kawaida (mduara ulio kushoto) hupungua ujazo (mduara ulio kulia), ambao huongeza uwezekano wa mivunjiko. Mifupa ya uti wa mgongo (pingili) inapopunguza uzito, zinaweza kulegea na kupinda. Mvunjiko huu unaitwa mvunjiko wa mgandamizo wa uti wa mgongo. Mapingili mengi ya mgongo yakivunjika, mpindo usio wa kawaida wa uti wa mgongo unaoitwa kibyongo cha dowager (kulia) unaweza kutokea.