Katika Chumba cha Upasuaji
Chumba cha upasuaji hutoa mazingira safi kabisa ambamo timu ya upasuaji inaweza kufanya upasuaji. Timu ya upasuaji inajumuisha wafuatao:
Daktari mkuu wa upasuaji: Huongoza upasuaji
Daktari msaidizi mmoja au zaidi wa upasuaji: Humsaidia daktari mkuu wa upasuaji
Mtaalam wa ganzi/nusukaputi: Hudhibiti utoaji wa dawa ya gazi na kufuatilia hali ya mtu kwa ukaribu
Muuguzi wa Kusaafisha: Humpatia zana daktari wa upasuaji
Muuguzi anayezunguka: Huipatia timu ya upasuaji zana za ziada
Kwa kawaida chumba cha upasuaji kina skrini inayoonyesha ishara za muhimu, meza ya kuweka zana, na taa ya upasuaji. Gesi za ganzi/nusukaputi huingizwa kwenye mashine ya ganzi kwa njia ya bomba. Katheta ambayo imeunganishwa kwenye mashine ya kunyonya huondoa damu ya ziada na majimaji mengine, ambayo yanaweza kumzuia daktari wa upasuaji kuona tishu vizuri. Majimaji yanayotolewa kupitia vena, huanza kabla ya mtu kuongia katika chumba cha upasuaji, na huendelea.