Sisti Fibrosisi: Si tu Ugonjwa wa Mapafu
Sisti fibrosisi huathiri mapafu na pia viungo vingine kadhaa.
Kwenye mapafu majimaji mazito yanazuia njia ndogo za hewa, ambayo inaambukizwa na kuwa na mwako. Kadiri ugonjwa unavyoendelea, kuta za bronchioli zinakuwa nene, njia za hewa zinajazwa majimaji yaliyoambukizwa, eneo la mapafu linapata maambukizi, na vinundu vya limfu vinapanuka.
Kwenye ini, majimaji mazito yanaziba mfereji wa nyongo. Mawe yanaweza kujitengeneza kwenye kibofu nyongo.
Kwenye kongosho, majimaji mazito yanaweza kuzuia tezi kabisa kiasi kwamba vimeng'enya haviwezi kufika kwenye utumbo mdogo. Kongosho linaweza kuzalisha insulini kidogo, kwa hivyo baadhi ya watu wanapata kisukari (kwa kawaida katika umri wa balehe au utu uzima).
Kwenye utumbo mdogo, mekoni ileus (aina ya kizuizi cha utumbo) unaweza kutokea kwa sababu ya majimaji mazito na unaweza kuhitajika kufanya upasuaji wa watoto waliozaliwa karibuni.
Viungo vya uzazi vinaathiriwa na sisti fibrosisi kwa namna mbalimbali, kwa kawaida kutokuwa na uwezo wa kutungisha mimba kwa wanaume.
Tezi za jasho kwenye ngozi zinatoa majimaji yenye chumvi zaidi kuliko kawaida.