Muhtasari wa Uchungu wa Uzazi na Kuzaa

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2024

Kujifungua mtoto huanza unapoanza kuhisi uchungu wa uzazi na ni pamoja na kujifungua mtoto wako na kondo la nyuma (kondo la uzazi).

Je, ninapaswa kufanya maamuzi gani kuhusiana na uchungu wa uzazi na kujifungua?

Kabla ya kupata mtoto, amua:

  • Unayetaka awe na wewe

  • Mahali ambapo unataka kujifungulia mtoto wako

  • Aina ya misaada ya maumivu unaweza kutaka wakati wa uchungu wa uzazi

Nani anapaswa kuwa nami?

Kwa kina mama wengi, kuongozana na mwezi wake au mtu mwingine wa kumsaidia kama vile doula, wakati wa uchungu wa uzazi wa uzazi ni jambo la muhimu. Kutiana moyo na kufarijiana kunaweza kupunguza wasiwasi.

Nijifungulie mtoto wangu wapi?

Unaweza kujifungulia mtoto wako katika:

  • Hospitali

  • Kituo cha kujitegemea cha kujifungua

  • Nyumbani

Hospitali zina madaktari, wauguzi, na vifaa vya kushughulikia matatizo yoyote yasiyotazamiwa ambayo wewe au mtoto wako anaweza kuwa nayo.

kituo cha kujifungulia ni kituo cha matibabu ambacho kina mazingira kama ya nyumbani kuliko hospitali. Huenda ikakuruhusu mabadiliko zaidi (kama vile kuruhusu wageni kila wakati au kukuruhusu uende nyumbani mapema). Baadhi ya vituo vya kujifungua viko hospitalini. Vituo vingine vya kujifungua ni vituo tofauti ambavyo vina mipango na hospitali za karibu ili kushughulikia matatizo yoyote.

Kujifungua nyumbanu ni kawaida katika nchi nyingi. Mtaalamu wa afya mwenye mafunzo na leseni anapaswa kuwepo wakati wa kujifungulia nyumbani. Kina mama wanaojifungua nyumbani wanapaswa kupanga kufika hospitalini ndani ya dakika 30 iwapo kuna matatizo. Katika baadhi ya nchi, wataalamu wa afya waliodhinishwa (kama vile wauguzi na wakunga walioidhinishwa) mara nyingi hawapatikani, na wakina mama hujifungua kwa msaada wa wakunga wasio na utaalamu au wakunga wa jadi.

Nitajitayarisha vipi kwa leba na kujifungua?

Kujifungua kwingi hufuata mtindo sawa. Ili kujifunza nini cha kutarajia katika kujifungua kwa kawaida, unaweza:

  • Fanya darasa la kujifungua, iwe peke yako au na mpenzi wako

  • Soma kuhusu uzazi (daktari au muuguzi wako anaweza kukupendekezea vitabu na tovuti nzuri)

  • Zungumza na wanawake wengine ambao wamejifungua