Mmenyuko wa Kuathiriwa na Mwanga

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga ni nini?

Mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga ni tatizo ambalo mfumo wa kingamwili wako huathirika kupita kiasi kutokana na mwanga wa jua. Mmenyuko huu wakati mwingine pia huitwa mzio wa jua.

  • Hisia kali za mwanga husababisha mabaka mekundu na kuwasha kwenye ngozi yako, kwa kawaida ngozi ambayo imekuwa kwenye mwanga wa jua

  • Dawa au kemikali fulani zinaweza kufanya ngozi yako kuwa nyeti kwa jua

  • Mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga unaweza kuwa wa kurithi katika familia

  • Baadhi ya magonjwa yanaweza kusababisha mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga

  • Mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga hutoweka wenyewe, lakini dawa mara nyingine husaidia kukuondolea hisia mbaya

Ni nini husababisha mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga?

Kuna aina tofauti za mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga ambazo zina sababishwa na vitu tofauti, pamoja na:

  • Zinazosababishwa na dawa fulani unazotumia

  • Zile zilizosababishwa na kemikali fulani ambazo ulikuwa umeathiriwa kwazo

  • Zile zilizosababishwa na magonjwa uliyo nayo (kama vile lupasi)

Angalau dawa na kemikali zisizopungua 100 zinajulikana kusababisha mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga.

Mara nyingi haionekani kuwa na sababu maalum, ingawa hisia kali kwa mwanga hutokana na hali ya kurithi katika familia.

Je, dalili za mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga ni zipi?

Dalili ni tofauti kulingana na aina ya mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga uliyo nayo. Unaweza kuwa na:

  • Uvimbe mwekundu unaowasha

  • Mabaka mekundu, yanayouma yenye kufanana na mbabuko wa ngozi utokanao na kuchomwa na jua

Dalili mara nyingi huonekana kwenye ngozi ambayo ilikuwa kwenye jua. Lakini aina moja ya mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga inaweza kuenea hadi kwenye ngozi ambayo haikuwa kwenye jua.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga?

Madaktari wanashuku mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga wakati una upele haswa kwenye maeneo ya ngozi yako iliyokuwa kwenye jua. Madaktari watakuuliza kuhusu dawa na vitu unavyotumia au kupaka kwenye ngozi yako.

Madaktari wanaweza kufanya vipimo, kama vile:

  • Vipimo vya vijisehemu vidogo vya ngozi kugundua viungo unavyoweza kuwa na mzio navyo

  • Kuangazia mwanga wa UV (ultraviolet) kwenye ngozi yako ili kuona ikiwa husababisha athari

Madaktari hutibu vipi mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga?

Matibabu ni tofauti kulingana na aina ya mmenyuko wa kuathiriwa na mwanga.

Madaktari watafanya:

  • Hukuambia usitishe utumiaji wa dawa au viungo vyovyote vinavyoongeza kuwa na hisia kali za mwanga

  • Watakupa kotikosteroidi za kupaka kwenye ngozi au kumeza

  • Kukupa dawa nyingine ikiwa athari ni za mara kwa mara au ni kali

Huenda madaktari pia wakakufanya:

  • Epuka kutumia muda mwingi kwenye mwanga wa jua

  • Vaa nguo za kujikinga unapotoka nje