Psoriasis ni nini?
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Psoriasis ni ugonjwa sugu (kudumu) wa ngozi ambao husababisha madoa mekundu kwenye ngozi yako. Mabaka yaliyotuna yanaweza kuwa na magamba ya rangi ya fedha.
Psoriasis imeenea sana na inaweza kurithishwa kwenye familia
Watu wenye ngozi yeupe wanapata psoriasis mara nyingi sana kuliko watu weye ngozi nyeusi
Psoriasis kwa kawaida inaanza unapouwa na umri kati ya miaka 16 hadi 22 au katika ya miaka 57 hadi 60
Mabaka yanaweza kuwa makubwa au madogo, na yanaweza kutokea sehemu yoyote kwenye mwili wako, hasa kwenye kope zako, magoti na ngozi ya kichwa
Psoriasis haiwezi kutibiwa, lakini mabaka yanaweza kuondoka kwa vipindi virefu vya muda kisha kurejea
Madaktari wanatibu psoriasis kwa kutumia tiba ya nuru (kuangaza mwangaza wa UV kwenye ngozi yako ili kuiponya) na dawa
Je, nini husababisha psoriasis?
Madaktari hawana uhakika ni nini hasa kinachosababisha psoriasis. Linaweza kuwa ni tatizo kwenye mfumo wa kingamaradhi (seli, tishu na viungo vinavyolinda mwili wako dhidi ya ugonjwa na maambukizi). Psoriasis hujitokeza katika familia. Hiyo ina maana kwamba ikiwa una psoriasis baadhi ya ndugu zako huenda wakawa na psoriasis pia.
Miibuko
Psoriasis ina kawaida ya kuja na kuondoka, ingawa baadhi ya mabaka huenda yasiondoke kabisa. Miibuko ni pale ambapo inarejea au inakuwa mbaya zaidi. Miibuko inaweza kuchochewa na:
Majeraha ya ngozi
Mbabuko wa ngozi unaotokana na jua
Maambukizi, kama vile mafua na koo lenye strep
Hali ya hewa ya msimu wa baridi
Kunywa pombe
Viwango vya juu vya msongo wa mawazo
Dawa fulani
Miibuko inatokea sana kwa watu ambao wana uzito mkubwa kupita kiasi, wanavuta tumbaku au wana maambukizi ya VVU.
Je, dalili za psoriasis ni zipi?
Mabaka ya ngozi moja au zaidi yaliyovimba, mekundu yakiwa na magamba ya rangi ya fedha kwenye ngozi ya kichwa, kope, magoti, mgongo wa chini, au matakoni.
Mabaka ya ngozi yanaweza kuonekana pia kwenye nyusi zako, kwapa, tumbo na kuzunguka njia ya haja kubwa au katikati ya matako yako
Wakati mwingine, kucha za vidole vyake zinaweza kuwa butu, nene na zina mwonekano mbaya
Mabaka ya ngozi yanaweza:
Kuondoka baada ya miezi kadhaa
Kubaki vilevile
Kuwa makubwa zaidi
Kukua kwenye sehemu nyingine ya mwili wako
Kuondaoka na yasirudi tena kwa miaka kadhaa
Madoa hayo yana mwasho au uchungu. Unaweza usumbuliwe kwa jinsi yanavyoonekana.
Baadhi ya watu wenye psoriasis wana dalili nyingine kama vile maungio yaliyovimba yenye maumivu au malengelenge yaliyojaa usaha.
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina psoriasis?
Kawaida daktari anaweza kubaini ikiwa una psoriasis kulingana na mwonekano wa ngozi yako. Ikiwa daktari hana uhakika, atachukua sampuli ya ngozi yako kuichunguza kwa kutumia hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi).
Je, madaktari hutibu vipi psoriasis?
Madaktari watakupatia aina moja ya matibabu au zaidi:
Dawa kuweka kwenye ngozi yako
Tiba ya nuru (kuweka mwangaza wa UV kwenye ngozi yako ili kuiponya)
Dawa zinazotolewa kama sindano au vidonge, baadhi ya hizi dawa zina madhara, kwa hivyo zinatumika tu kutibu psoriasis ikiwa mbaya zaidi.