Nyenzo za Mada
Vigaga ni nini?
Vigaga ni upele unaowasha. Unasababishwa na wadudu wadogo wanaoitwa utitiri.
Utitiri unaingia kwenye ngozi yako na unataga mayai
Utitiri unaenea kwa urahisi kwa kukutana na watu kimwili
Upele unawasha vibaya sana
Madaktari wanatibu vigaga kwa kutumia krimu yenye dawa
Picha kwa hisani ya Karen McKoy, MD.
Nini kinachosababisha vigaga?
Vigaga vinasababishwa na aina fulani ya utitiri. Utitiri unaingia kwenye ngozi yako ili kutaga mayai. Hali hii inasababisha mwasho mkali na upele.
Unaweza kupata vigaga kwa kugusana na mtu mwenye vigaga. Unaweza pia kupata vigaga kwa kutumia taulp, matandiko au n guo zilizotumiwa na mtu mwenye vigaga.
Dalili za vigaga ni zipi?
Mwasho mkali ambao kwa kawaida unakuwa mbaya wakati wa usiku
Upele wenye vivimbe vidogo byekundu ambavyo wakati mwingine vinaunda mstari ulionyooka
Vivimbe hivi kwa kawaida huwa vinakuwa kwenye vidole, vifundo na mikono lakini vinaweza kuwa sehemu yoyote kwenye mwili wako (isipokuwa kwenye uso wa mtu mzima)
Watoto wachanga wanaweza pia kupata upele kwenye uso wao, ngozi ya kichwa (hasa nyuma ya masikio), viganja vya mikono yao au makanyagio ya miguu yao
Watu wazima wanaweza kuwa na upele mdogo sana, na kufanya iwe vigumu kuona
Ikiwa una maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, vigaga vinaweza kuenea kwenye mwili wako wote
Madaktari wanawezaje kujua kama nina vigaga?
Madaktari wanaweza kujua kulingana na dalili zako na kwa kuangalia upele ulio nao
Wakati mwingine, madaktari watapasua kivimbe 1 au 2
Watachunguza majimaji kwa kutumia hadubini ili kuona utitiri
Madaktari wanatibu vipi vigaga?
Madaktari watakutibu, wanafamilia wako na mtu yeyote ambaye amekutana na wewe.
Ili kuua utitiri
Watu wazima and watoto wenye umri wa miaka 2 na zaidi:
Weka krimu ya dawa iliyopendekezwa na daktari wako katika mwili wako wote kuanzia kwenye shingo
Isafishe baada ya saa 8 hadi 14
Kwa watoto wachanga chini ya miaka 2:
Weka krimu tofauti ya dawa iliyopendekezwa na daktari wako katika mwili wa mtoto na kichwa
Krimu haipaswi kwenda kwenye ngozi kuzunguka macho ya mtoto na kinywa
Krimu inapaswa kwenda kwenye mikunyo ya ngozi ya mtoto, kwenye kucha za vidole na kucha za vidole vya miguuni na chini ya tumbo
Watu wenye vigaga vyenye hali mbaya au mfumo wa kingamaradhi ambao ni dhaifu wanaweza kuhitaji kutumia dawa kwa kinywa.
Baada ya utitiri kuuawa, bado unaweza kuendelea kuwa na mwasho na vivimbe kwa hadi wiki 3 zaidi. Huenda madaktari wakakufanya:
Weka kiasi kidogo cha krimu yenye dawa kwenye upele au tumia dawa kwa kinywa ili kusaidia kupunguza mwasho
Tumia dawa za kuua bakteria ikiwa umepata maambukizi ya ngozi kwa kukuna sana ngozi yako
Ninawezaje kuzuia vigaga visienee?
Utitiri unasambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, wakati mwingine kila mtu kwenye familia. Ili kuzuia vigaga visienee:
Mwone daktari mara tu utakapokuwa na dalili
Madaktari watakutibu, wanafamilia wako na mtu yeyote ambaye amekutana (ikiwa ni pamoja na kukutana kingono) na wewe
Pia, ua utitiri ambao unaweza kuwa kwenye nguo zako, mataulo na matandiko kwa kufanya moja kati ya haya yafuatayo:
Zifue kwa maji moto na uzikaushe kwenye joto
Peleka zifuliwe na wataalamu
Ziweke kwenye mfuko wa plastiki uliofungwa kwa angalau siku 3 ili utitiri ufe
Watu wengi wanapata vigaga katika eneo ambapo kuna watu wengi sana, kama vile shule au kwenye jeshi. Kupata vigaga hakuhusiani na kuwa mchafu.