Majeraha ya Tishu Yasiyo ya Kuganda

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2022

Majeraha ya tishu yasiyo ya kuganda ni nini?

Majeraha ya tishu yasiyo ya kuganda ni majeraha ya ngozi yaliyosababishwa na baridi. Ikiwa ngozi yako itapata baridi kali itaganda, hii hujulikana kama ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi. Aina za kawaida za majeraha ya tishu yasiyo ya kuganda ni:

  • Frostnip

  • Ugonjwa unaotokana na majimaji au baridi miguuni (Trench Foot)

  • Ugonjwa wa Chilblains

Frostnip

Frostnip ni jeraha ambalo ngozi yako hupata baridi kali na hivyo kupata ganzi, kuvimba na kuwa nyekundu.

  • Tibu frostnip kwa kupasha joto sehemu hiyo kwa dakika chache

  • Sehemu hiyo itauma na kuwasha pale inapopata joto

  • Wakati mwingine, sehemu hiyo inaweza kuwa yenye kuathiriwa na baridi kwa muda mrefu baada ya hapo

Ugonjwa unaotokana na majimaji au baridi miguuni (Trench Foot)

Tumbukio la mguu ni jeraha litokanalo na kuvaa soksi au viatu vilivyolowa, vyenye ubaridi. Mara nyingine huitwa ufuo wa mguu.

  • Mguu wako hupauka, na kuwa na unyevunyevu, huvimba, kupata ganzi na baridi

  • Ili kutibu tumbukio la mguu, pasha joto kwa taratibu, kausha na unyanyue mguu wako

  • Mguu wako utabadilika rangi na kuwa mwekundu na wenye maumivu utakapoanza kupata joto na pia unaweza kupata malengelenge

  • Wiki zinazofuata, mguu wako unaweza kuwa unahisi kwa haraka na kujaa jasho

  • Madaktari wanaweza kukupatia dawa za kuua bakteria ili kuzuia maambukizi

Zuia tumbukio la mguu kwa:

  • Kuvaa viatu na buti zinazokutosha vizuri

  • Kubadilisha soksi zako kila siku

  • Kuweka miguu yako katika hali ya ukavu

Ugonjwa wa Chilblains

Uvimbe unaotokana na baridi kali ni sehemu za ngozi yako zenye kuwasha, nyekundu au zinazovimba kutokana na kukaa kwenye hali ya hewa yenye baridi kavu.

  • Uvimbe unaotokana na baridi kali ni nadra kutokea lakini si hatarishi

  • Unapata mwasho, maumivu, wekundu na wakati mwingine malengelenge, hasa kwenye vidole vyako vya mikono au sehemu za mbele za miguu yako

  • Tibu uvimbe unaotokana na baridi kwa kuepuka kukaa kwenye baridi

  • Kuepuka nikotini kunaweza kusaidia kuzuia uvimbe unaotokana na baridi