Kidonda kwenye konea

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, kidonda kwenye konea ni nini? 

Konea yako ni safu ya wazi mbele ya jicho lako. Kidonda kwenye konea ni jeraha lililo wazi kwenye konea yako.

Mtazamo wa Ndani wa Jicho

  • Kwa kawaida vidonda kwenye konea husababishwa na maambukizi

  • Maambukizi yanaweza kuanza kwa jeraha au kuchubuka kwa jicho, mwasho utokanao na lenzi za kupachika, au magonjwa fulani ya macho

  • Unaweza kuwa na maumivu ya macho, machozi, hisia kali kwa mwanga, na macho mekundu, yenye mabaka ya damu

  • Kwa kawaida madaktari hutibu vidonda kwenye konea kwa kutumia matone ya macho ya dawa za kuua bakteria

  • Wakati fulani baada ya kidonda kwenye konea kupona, konea yako hubaki na jeraha la ukungu ambalo huathiri uwezo wako wa kuona

Muone daktari mara moja ikiwa unafikiri kuwa una kidonda kwenye konea kwa sababu kinaweza kusabisha upofu.

Je, nini husababisha vidonda vya konea?

Vidonda vingi vya konea husababishwa na:

  • Maambukizi

Bakteria, virusi na vimelea wengi wanaweza kuhusika

Kwa kawaida, pia unakuwa na tatizo la jicho ambalo huongeza uwezekano wa kupata maambukizi, kwa mfano:

Je, dalili za kidonda kwenye konea ni zipi?

Kwa kawaida, kidonda kwenye konea hutokea kwenye jicho moja tu.

Dalili za kidonda kwenye konea ni pamoja na:

  • Macho mekundu, yaliyojaa machozi, yenye madoa ya damu

  • Maumivu ya macho

  • Kuhisi kama vile kitu kimekuingia machoni

  • Mwanga huumiza jicho lako

  • Doa jeupe au la kijivu kwenye jicho lako

Iwapo kidonda kwenye konea hakitatibiwa, kinaweza kuchimba, na maambukizi yanaweza kusambaa kwenye jicho lako lingine.

Wakati mwingine unabaki na kovu baada ya kidonda kwenye konea kupona. Kovu linaweza kuathiri uwezo wako wa kuona.

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina kidonda kwenye konea?

Madaktari hutambua uwepo wa kidonda kwenye konea kwa kutazama jicho lako. Watafanya uchunguzi kamili wa jicho, ikijumuisha kukagua uwezo wako wa kuona, na wanaweza pia:

  • Kuondoa sampuli ya kidonda kwenye konea kwa ajili ya upimaji

Je, madaktari hutibu vipi vidonda vya konea?

Kidonda cha konea kinaweza kusababisha upofu, hivyo ni muhimu kuonana na daktari mara moja ikiwa unadhani kuwa una kidonda cha konea.

Madaktari watakutibu mara moja kwa:

  • Matone ya macho ya dawa za kuua bakteria ili kupambana na maambukizi

  • Matone ya macho ya kutanua macho yako, ambayo hukusaidia kupunguza maumivu

Unaweza kuhitajika kutumia matone ya macho ya dawa za kuua bakteria kila baada ya saa au saa mbili kwanza.

Kwa nadra, ikiwa kovu litaathiri uwezo wako wa kuona, madaktari wanaweza kufanya upandikizaji wa konea (upasuaji wa kuondoa konea yenye ukungu na kuibadilisha na ile yenye afya, iliyo safi)