Kuvimba kwa Konea

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, kuvimba kwa konea ni nini? 

Konea yako ni safu ya wazi mbele ya jicho lako. Kuvimba kwa konea ni uchungu wenye kukera kwenye konea yako.

Mtazamo wa Ndani wa Jicho

  • Kuvimba kwa konea hufanya macho yako kuwa mekundu na kuuma sana

  • Mwanga mkali huumiza, na kuona kwako kunaweza kuwa na hali ya ukungu

  • Madaktari hutibu kuvimba kwa konea kwa namna tofauti kutegemea na chanzo chake

  • Unaweza kuhitaji matone ya macho ya dawa za kuua bakteria au dawa ya kupaka

Uvimbe wa konea mbaya unaweza kusababisha jeraha kwenye konea (kidonda kwenye konea), hali ambayo ni ya dharura kwa sababu inaweza kusababisha upofu.

Je, nini husababisha kuvimba kwa konea?

Sababu za kuvimba kwa konea ni pamoja na:

  • Maambukizi ya macho

  • Kemikali kuingia kwenye jicho lako, ikijumuisha baadhi ya dawa za macho

  • Kiasi kikubwa cha nuru ya urujuani, kama vile inayotokana na kuchomela au mwanga mkali wa jua

  • Kuvaa lenzi za kupachika kwa muda mrefu au kutozisafisha vizuri

  • Macho makavu

Je, dalili za kuvimba kwa konea ni zipi?

Dalili zinajumuisha:

  • Macho mekundu, yaliyojaa machozi, yenye madoa ya damu

  • Maumivu au kuungua, hisia ya uchafu machoni pako

  • Mwanga huumiza macho lako

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina uvimbe wa konea?

Madaktari hutambua uwepo wa vidonda kwenye konea kwa kutazama macho yako. Watafanya:

  • Uchunguzi kamili wa jicho, ikijumuisha kupima uwezo wako wa kuona

Je, madaktari hutibu vipi kuvimba kwa konea?

Matibabu hutegemea chanzo cha kuvimba huko:

  • Matone ya jicho ya dawa za kuua bakteria iwapo una maambukizi

  • Machozi bandia au dawa za kupaka zenye kulainisha iwapo una macho makavu

  • Wakati mwingine matone ya macho ili kupanua macho yako, hali ambayo hupunguza maumivu

Pia madaktari watakufanya ujiepushe na chochote ambacho kinaweza kuwa kimesababisha kuvimba kwa macho, kama vile kuzingatia tahadhari za usalama wakati wa kuchomelea au kutumia kemikali. Ikiwa utavaa lenzi za kupachika, madaktari watahakikisha unazitumia na kuzisafisha kama inavyotakiwa.