Sumu ya Chakula ya Staphylococcal

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Je, sumu ya chakula ya staphylococcal ni nini?

Sumu ya chakula ni tatizo ambalo kitu unachokula hukupa kuharisha na kukufanya utapike. Staphylococci ni aina ya bakteria (vijidudu). Kwa hivyo, sumu ya chakula ya staphylococcali ni unapougua kutokana na kula chakula ambacho kina aina hii ya bakteria inayokua ndani yake Bakteria hii hutengeneza toksini (sumu). Ni sumu hizi wala si bakteria zinazokufanya kuwa mgonjwa.

Aina nyingine za bakteria zinaweza pia kusababisha sumu ya chakula. Kwa mfano, sumu ya chakula ya klostridiali husababishwa na bakteria wanaoitwa klostridia.

Vyakula vinavyoweza kukupa sumu ya chakula ya staphylococcal vinaweza kunukia na kuonja kawaida. Vyakula vingi vinaweza kusababisha sumu ya chakula ya staphylococcal, hasa vyakula ambavyo vilikuwa:

  • Havijapikwa kwa muda mrefu wa kutosha

  • Vimeachwa vikiwa nje ya jokofu kwa joto la kawaida

  • Vimeshikwa na mtu ambaye ana maambukizi ya ngozi ya staphylococcal

Sumu ya chakula inafanana sana na gastroenteraitisi. Lakini katika gastroenteraitisi, vijidudu katika chakula hukua ndani ya tumbo lako na kukufanya kuwa mgonjwa. Vijidudu hivyo havitengenezi sumu.

Je, dalili za sumu ya chakula ya staphylococcal ni zipi?

Kwa kawaida dalili huanza ghafla sana masaa 2 hadi 8 baada ya kula na ni pamoja na:

  • Kuhisi mgonjwa sana kwenye tumbo lako

  • Kutapika

  • Kukakamaa kwa tumbo

  • Kuharisha

Kwa kawaida dalili hudumu kwa takriban saa 12. Hutoweka haraka kama zilivyokuja. Hata hivyo, ikiwa hunywi majimaji ya kutosha, unaweza kujihisi dhaifu kwa muda mrefu zaidi.

Sumu ya chakula ya Staphylococcal inaweza kuwa ya kutishia maisha ya watoto wachanga na watoto wadogo, watu wazima wenye umri mkubwa sana, na watu walio na matatizo ya kiafya ya muda mrefu.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina sumu ya chakula ya staphylococcal?

Madaktari wanashuku sumu ya chakula ya staphylococcal kulingana na dalili zako, haswa ikiwa watu waliokula chakula sawa na wewe waliugua pia. Madaktari huwa hawafanyi vipimo kwa kawaida, lakini wakati mwingine hupima mabaki ya chakula kwa ajili ya kutafuta bakteria ya staphyloccocal.

Je, madaktari hutibu vipi sumu ya chakula ya staphylococcal?

Madaktari watafanya:

  • Atakueleza unywe vinywaji kwa wingi

Ikiwa dalili zako ni kali, huenda daktari:

  • Watakupa dawa ya kukufanya uache kujihisi mgonjwa tumboni mwako na kutapika

  • Watakupa majimaji kupitia mshipa wako wa damu (IV)

Dawa ambayo inaweza kuzuia kutapika huwa inatolewa kama sindano au dawa ya kuingizwa kwenye tundu la haja kubwa. Dawa ya kuingizwa kwenye tundu la haja kubwa ni tembe inayoyeyuka ambayo huwekwa kwenye rektamu yako.

Je, ninawezaje kuzuia sumu ya chakula ya staphylococcal?

Pika na uhifadhi chakula kwa usalama:

  • Usiandae chakula ikiwa una maambukizi ya ngozi

  • Kula chakula mara tu ukimaliza kukikiandaa

  • Pika chakula (kama vile nyama) ipasavyo ili kufikia viwango vya joto vilivyo salama

  • Weka chakula kilichobaki kwenye jokofu

  • Usiweke chakula kilichoandaliwa katika joto la kawaida