Vipimo Vinavyohusiana na Asidi na Vinavyohusiana na Refluksi

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Tumbo yako hutengeneza asidi za kusaidia kusaga vyakula.

Refluksi ya asidi ni wakati asidi ya tumbo inarudi juu kupitia kwenye umio kuelekea kwenye koo. Umio ni mrija unaounganisha koo na tumbo lako. Refluksi za asidi zinaweza kusababisha maumivu ya mwasho kwenye tumbo ya juu na kifua chako. Maumivu hayo wakati mwingine yanaitwa kiungulia.

Refluksi ya asidi pia inaitwa GERD (ugonjwa wa refluksi gastroesofajia).

Umio

Je, vipimo vya refluksi ya asidi ni vipi?

Madaktari huweka vifaa kwenye umio wako ili kupima kiwango cha asidi kilicho kwenye umio wako. Kuna aina 2 za vipimo:

  • Ufuatiliaji unaotegemea katheta, ambao unatumia bomba inayopinda (katheta) ili kupima asidi

  • Ufuatiliaji pasiwaya, ambao hutumia kapsuli ya redio kupima asidi

Kwa kipimo chochote, hauwezi kula au kunywa chochote baada ya usiku katikati kabla ya kipimo, lakini unaweza kula na kunywa kama kawaida wakati vifaa hivyo viko kwenye umio wako.

Vipimo hivi ni salama kabisa.

Ufuatiliaji unaotegemea katheta

  • Daktari wako huweka bomba nyembamba ya plastiki (katheta) kupitia kwenye pua na koo yako na chini kwenye umio wako

  • Bomba lina probu ambayo hutambua asidi

  • Bomba hukaa kwenye umio wako kwa saa 24 huku ukifuatilia dalili, milo na usingizi wako kwenye shajara

  • Waya zilizo ndani ya bomba hutuma maelezo kuhusu asidi kwenye umio wako kwenye rekoda

  • Daktari wako hulinganisha maelezo hayo kutoka kwenye rekoda na shajara yako ili kuona kama dalili zako zilitokea wakati asidi ilikuwa kwenye umio wako

Baadhi ya katheta zinaweza pia kupima vitu vingine kama makasi yanayopita kuelekea kwenye umio wako.

Ufuatiliaji pasiwaya

  • Baada ya kukupatia dawa ili kufanya upate usingizi, daktari wako hupitisha bomba ya kutazama inayopinda kupitia kwenye mdomo wako ili kuambatisha kapsuli ya kupima asidi kwenye sehemu ya chini ya umio wako

  • Unarekodi dalili, milo na usingizi wako kwenye shajara

  • Kapsuli hupima asidi kwenye umio wako na hutuma maelezo hayo kwa njia ya pasiwaya kwenye kipokeaji unachovalia

  • Daktari wako hulinganisha maelezo na shajara yako ili kuona kama dalili zako zilitokea wakati asidi ilikuwa kwenye umio wako

  • Kapsuli hio huanguka ndani ya wiki na hupita kwenye utumbo wako na kutoka kwenye mwili wako kwenye kinyesi chako