Je, kifo cha mtoto huathirije familia?
Kumpoteza mtoto ni jambo gumu sana na la kuumiza kwa familia.
Wazazi walio na majonzi ya kufiwa wanaweza kuwa na wakati mgumu wa kukidhi mahitaji ya watoto waliosalia
Wakati mwingine wazazi hupata mtoto mwingine kwa haraka ili “achukue nafasi” ya mtoto aliyeaga—katika hali kama hizi, wazazi wanaweza kumlinda mtoto huyo kupita kiasi au wawe na wakati mgumu wa kujenga uhusiano wa karibu naye
Huenda usaidizi wa ushauri nasaha ukafaa
Huenda kukawa na kikundi cha usaidizi kwenye jamii yako cha wazazi waliofiwa na mtoto
Ninawezaje kuelezea watoto kuhusu kifo cha mwanafamilia au mpendwa?
Wape watoto ufafanuzi rahisi katika kiwango ambacho wanaweza kuelewa
Watoto wakubwa wanaweza kuelewa zaidi—waruhusu wajue kwamba ni kawaida kuwa na udadisi na kuuliza maswali
Usilinganishe kifo na hali ya kulala na kukosa kuamka kamwe kwa sababu watoto wanaweza kuogopa wakati wa kulala
Mtoto wako akionyesha huzuni kubwa au akijitenga, akiacha kushiriki katika shughuli, au akianza kuwa mbishi, mpeleke mtoto kwa mshauri wa kisaikolojia ili apate usaidizi.
Je, watoto wanapaswa kuwatembelea watu wagonjwa au wanaofariki hospitalini?
Unaweza kumuuliza daktari wa mtoto wako iwapo unaweza kumruhusu mtoto wako kumtembelea mtu mgonjwa sana au anayefariki, iwe mtu huyo ni mtoto au mtu mzima.
Waandae watoto kwa ajili ya matembezi hayo:
Fafanua kuwa mtu huyo huenda akaonekana tofauti lakini ni mtu yule yule
Mwandae mtoto kuhusiana na hali ya mabadiliko ya mwili, kama vile kupoteza au kuongeza uzani au kupoteza nywele
Waandae watoto kuhusiana na vifaa vya matibabu ambavyo wanaweza kuona
Je, watoto wanaweza kuhudhuria mazishi ya mpendwa wao?
Huu ni uamuzi binafsi. Iwapo watoto watahudhuria mazishi, hakikisha kuna mtu pamoja nao wa kuangazia mahitaji yao na kuwaruhusu waondoke wakipenda.
Waambie watoto kuwa ni sawa kuuliza maswali kuhusu kifo na kufa.
Wape watoto njia ya kusaidia. Wanaweza:
Kuandika au kuchora kadi
Kuchuma maua
Kufunga zawadi
Kukusanya chakula, pesa au vifaa vya kuchezea