Karibu katika Tovuti ya Miongozo ya MSD kwa Kiswahili
Maoni21/10/24 Sandy J. Falk, MD

Tunafurahi kuwakaribisha wasomaji wa Kiswahili kwenye tafsiri hii mpya kabisa ya Miongozo ya MSD, Toleo la Vidokezo vya Haraka.

Tovuti za miongozo ni toleo la sasa la kidijitali la mwongozo wa tiba kwa ajili ya wataalamu wa huduma za afya. Mwongozo huu ulichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1899, ukawa kitabu kirefu zaidi cha tiba kilichoendelea kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza. Kwa miaka mingi, familia nyingi zilikuwa na nakala ya Mwongozo wa kitaalamu nyumbani na ulitumika kama chanzo muhimu cha taarifa za tiba ili kusaidia kuelewa na kujali afya zao. Mnamo mwaka 1997, Kitabu cha Kiada cha kwanza cha Afya ya Nyumbani kilichapishwa, toleo la Mwongozo lililoundwa mahususi kwa ajili ya wagonjwa, walezi na watumiaji wote wa huduma za afya.

Toleo la Miongozo ya MSD la Vidokezo vya Haraka, ni sehemu ya Toleo la Mtumiaji, ni nyenzo ya kidijitali ya taarifa za afya inayojumuisha taarifa mbalimbali kuhusu maelfu ya magonjwa na matibabu katika nyanja zote za tiba. Mwongozo umeandaliwa kuwa sehemu ya kwanza bora zaidi ya kwenda kujifunza kuelewa na kuhudumia afya ya binadamu. Toleo la Mtumiaji linawasilisha taarifa ile ile inayoaminika ambayo inapatikana kwa wataalamu wa tiba katika lugha dhahiri, ambayo ni rahisi kueleweka ikiambatana na vielelezo, video na picha nyingi. Kwa kuwasaidia watu kuelewa zaidi kuhusu afya zao na afya ya familia na marafiki, ni matumaini yetu kuwa tutaunga mkono afya na ustawi na kuwapa watu maarifa ya kuelewa afya zao, kuwasiliana kwa ufanisi na madaktari wao na kufanya maamuzi sahihi kuhusu tiba.

Maudhui ya Mwongozo yameandikwa na mamia ya wataalamu wa tiba duniani kote na lugha na matoleo yote ya tovuti yanapatikana bila malipo, bila matangazo au ujumbe wa biashara.

Tafadhali tembelea tovuti hii mara kwa mara ili ujue kilichobadilika na kusoma maudhui mapya, kuwa huru kuwasiliana nasi ukiwa na maoni au maswali yoyote. 
Sandy Falk, MD