Kuganda ngozi

Kukaa kwenye halijoto ya baridi la kuganda kunaweza kuharibu au kufanya tishu za nje kabisa zipate ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi, kama vile mikono, miguu, pua na masikio Hatua ya kwanza ya ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi inaitwa frostnip, ambayo huanza pale ngozi inapobadilika kuwa nyeupe na laini unapoigusa. Kwa kuendelea kukaa kwenye baridi, frostnip ya juujuu inaweza kutokea. Wakati huu, chembechembe za barafu hujiumba kwenye seli za ngozi: Matabaka ya chini zaidi ya ngozi yanaweza pia kuathirika. Hali ya baridi ikiongezeka, mishipa ya damu ya juujuu huganda, hivyo kupunguza mtiririko wa damu kwenye maeneo yaliyoathiriwa. Upungufu wa usambazaji wa damu na halijoto yenye barafu vinaweza kuanza kuleta athari kwa misuli, kano, mishipa, neva na hata mifupa iliyo chini. Seli zilizoganda hupoteza maji kwa haraka, na hivyo kuzidisha uharibifu wa tishu. Kiwango cha uharibifu wa kudumu wa tishu utategemea kiasi cha muda ambao tishu zilibaki zikiwa zimeganda. Matatizo fulani ya kiafya na dawa zinaweza kuongeza urahisi wa mtu kupata ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi. Ikiwa unadhani una ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi, pasha ngozi joto kwa taratibu kwenye maji ya uvuguvugu. Usitumie maji ya moto au joto kavu kupasha sehemu hiyo, kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kuzidisha uharibifu Uangalizi wa tabibu au mtaalamu wa afya ni wa muhimu katika kutibu ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi.