Muhtasari kuhusu Mfumo wa Uzazi wa Mwanaume

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, mfumo wa uzazi wa mwanaume ni nini?

Mfumo wa uzazi wa mwanaume ni mfumo kwenye mwili wa mwanaume wenye lengo la kuumba watoto. Baadhi ya viungo vya mfumo wa uzazi wa mwanaume, kama vile uume na njia ya mkojo, viko kwenye mfumo wa mkojo pia. Mfumo wa mkojo hutengeneza mkojo na kuutoa nje ya mwili.

Mfumo wa uzazi wa mwanaume ni pamoja na:

  • Korodani: Korodani mbili ndani ya mfuko wa pumbu hutengeneza manii na testosteroni, homoni ya ngono ya kiume

  • Epididimisi: Ogani ambayo imeunganishwa na korodani ambapo shahawa hukusanywa na kukomaa

  • Mfereji wa manii: Bomba linalosafirisha shahawa kutoka kwenye epididimisi hadi kwenye uume

  • Vilengelenge vya manii na tezi dume: Ogani zinazounda majimaji ya manii

  • Mrija wa mkojo: Bomba ambalo hubeba mkojo na manii kupitia uume

  • Uume: Ogani ya ngono ya mwanaume ambayo hujaa damu wakati anaposisimka kingono, hivyo kusababisha uume kusimika

Male Reproductive Organs

Je, mfumo wa uzazi wa mwanaume hufanyaje kazi?

Kazi kuu ya mfumo wa uzazi wa mwanaume ni pamoja na:

  • Kubalehe: Kuandaa mwili wako kwa ajili ya kuzalisha shahawa na kufanya ngono

  • Uume kusimika: Kufanya uume kuwa mgumu ili uweze kufanya ngono

  • Kumwaga manii: Kuachia manii

Je, shahawa na manii ni nini?

  • Shahawa ni seli za ngono za kiume, ambazo zinaweza kurutubisha yai la mwanamke na kuanzisha ujauzito

  • Manii ni uwoevu ambayo ina shahawa na hutoka kwenye uume wako wakati unapomwaga

Korodani zako hutengeneza mamilioni ya shahawa, ambazo huenda kwenye epididimisi ili zikakomae. Kisha husafiri kupitia bomba refu linaloitwa mfereji wa manii wakati zikielekea kwenye mrija wa mkojo na kutoka nje ya uume.

Manii zimeundwa na shahawa na kiasi kikubwa cha kioevu ambacho hurutubisha na kusafirisha shahawa. Kioevu huzalishwa na vilengelenge vya manii na tezi dume na huchanganyika na shahawa wakati wa kumwaga.

Je, uume kusimika ni nini?

Uume kusimika ni pale uume unapokuwa mkubwa na mgumu (kudinda). Uume kusimika hutokea pale unapokuwa umesisimka kingono na husababishwa na sababu za kimwili na kiakili.

Wakati wa uume kusimika, nafasi zilizo ndani ya uume wako hujaa damu, na kufanya uume urefuke, upanuke, na kuwa thabiti zaidi. Uume wako hujaa damu kwa sababu ateri ambazo huleta damu katika uume hupanuka ili damu itiririke ndani, na vena hubana ili kupunguza kiasi cha damu kinachotoka.

Je, kumwaga manii ni nini?

Kumwaga manii ni kutoa manii kwenye uume wako. Kusisimka kingono husababisha mshindo (kilele cha msisimko wa kingono) Wakati wa mshindo, misuli hubana na kusukuma manii kwenye mrija wa mkojo na kuzitoa nje ya uume.

Je, nini hutokea baada ya mshindo?

Baada ya mshindo kutokea au ikiwa msisimko wa kingono utakoma, damu zaidi hutiririka nje ya uume wako au kiasi kidogo cha damu huingia, hivyo kusababisha uume kulegea. Usimikaji mwingine wa uume hauwezi kutokea kwa muda fulani, mara nyingi takribani dakika 20 katika vijana.

Je, ni matatizo gani yanayoweza kuukumba mfumo wa uzazi wa mwanaume?

Baadhi ya matatizo ya mfumo wa uzazi wa mwanaume yanahusisha homoni, kwa mfano:

Matatizo mengine ya mfumo wa uzazi ni pamoja na:

Magonjwa mengi, kama vile maambukizi na saratani, yanaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.