Kuumwa na nyoka

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Nyoka wenye sumu na wasio na sumu huwauma watu. Nyoka wenye sumu wanaweza kuingiza sumu ya nyoka (sumu) pale wanapouma. Nchini Marekani, watu hufa kwa nadra kutokana na kuumwa na nyoka. Nchi zingine zina nyoka tofauti wenye sumu ambao huua watu wengi.

Ni aina chache tu za nyoka wenye sumu huishi nchini Marikani:

  • Wale wa kawaida zaidi: nyoka wa shimo, kama vile, nyoka-kayamba, nyoka mwenye kichwa cha rangi ya shaba, na nyoka mwenye mdomo unaofanana na pamba

  • Walio nadra: Nyoka ya matumbawe

Visa vingi vya kuumwa na nyoka wenye sumu husababishwa na nyoka-kayamba. Visa vya kuumwa na nyoka wa matumbawe ni nadra sana.

Je, dalili za kuumwa na nyoka ni zipi?

Kuumwa na nyoka asiye na sumu husababisha majeraha madogo ya kutobolewa ambayo yana uchungu kidogo. Hata hivyo, ikiwa unaogopa kuumwa, unaweza kupumua haraka, kuhisi kutokwa na jasho na maumivu tumboni mwako, na kuhisi moyo wako ukidunda. Dalili hizi zinaweza kukufanya ufikiri kuwa umeumwa na nyoka aliye na sumu.

Kuumwa na nyoka aliye na sumu husababisha dalili tofauti kulingana na:

  • Aina ya nyoka

  • Ukubwa wa nyoka (nyoka wakubwa huwa na sumu nyingi zaidi)

  • Kiasi cha sumu iliyodungiwa na (nyoka anaweza kudungia viwango tofauti vya sumu akikuuma)

  • Uliumwa sehemu gani ya mwili

  • Umri wako, ukubwa na afya yako

Dalili za kuumwa na nyoka wa shimo mwenye sumu

Sio nyoka wote wa shimo ambao wana sumu. Ikiwa kidonda hakiumi au kuvimba katika dakika 30 hadi 60 za kwanza, kuna uwezekano kuwa haukupata sumu yoyote. Ikiwa kidonda kinatoa maji, hiyo inaweza kuwa ishara ya sumu.

Baada ya kuumwa na nyoka wa shimo aliye na sumu, utakuwa na:

  • Uwekundu na uvimbe, takriban dakika 30 hadi 60 baada ya kuumwa

  • Michubuko na kubanwa, itaonekana masaa 3 hadi 6 baada ya kuumwa

  • Malengelenge yaliyojaa damu karibu na sehemu ulipoumwa

Unaweza kupata uvimbe mkubwa. Uvimbe kawaida huendelea kuwa mbaya zaidi kwa siku kadhaa.

Ikiwa ulidungwa sumu nyingi, unaweza pia kuwa na:

  • Udhaifu na kuchanganyikiwa

  • Kichefuchefu (kuhisi mgonjwa tumboni) na kutapika (kutapika)

  • Fizi kuvuja damu

  • Damu kwenye matapishi, kinyesi (kinyesi), au mkojo

  • Matatizo ya kupumua, haswa ikiwa nyoka-kayamba wa Mojave amekuuma

Masaa kadhaa baadaye, unaweza kuhisi

  • Maumivu ya kichwa

  • Uoni hafifu

  • Kope inayoinama

  • Mdomo mkavu

  • Kuwashwa, kufa ganzi, au ladha ya chuma kinywani mwako, ikiwa uliumwa na nyoka-kayamba

Dalili za kuumwa na nyoka wa matumbawe

  • Maumivu kidogo au kukosa kuwa na maumivu au uvimbe karibu na sehemu ulipoumwa

  • Baada ya masaa kadhaa, kidonda kinaweza kuwasha

  • Udhaifu wa misuli, ambao unazidi baada ya muda mrefu

Huenda pia:

  • Uoni hafifu au kuona vitu mara mbili

  • Udhaifu na kuchanganyikiwa

  • Kupumua kwa shida

  • Matatizo ya kuzungumza au kumeza

Je, ninapaswa kufanya nini nikiumwa na nyoka?

Ikiwa umeumwa na nyoka na una dalili, nenda hospitalini mara moja. Wakati unasubiri kupokea matibabu:

  • Ondoka mahali nyoka alipo

  • Weka mkono au mguu ulioumwa chini ya kiwango cha moyo wako

  • Jaribu kuwa mtulivu na utulie

  • Vua vito na nguo zinazobana kutoka kwenye sehemu uliyoumwa

Mambo ambayo hupaswi kufanya:

  • Usikate sehemu uliyoumwa au kunyonya sehemu ya uliyoumwa ili kujaribu kutoa sumu (haifanyi kazi)

  • Usitumie pakiti ya barafu (ina madhara)

  • Usifunge na mpira au kifaa cha kuzuia mtiririko wa damu kinachobana (kina madhara)

  • Usijaribu kumkamata nyoka ili kumpeleka kwa daktari (ikiwa nyoka amefariki, picha kwa kutumia simu inaweza kusaidia)

Ikiwa huduma ya afya iko mbali sana (kama wakati uko nje kukita kambi) na hauna dalili zozote, osha sehemu uliyong'atwa kwa kutumia sabuni na maji. Angalia ishara za maambukizi kama ambavyo ungefanya kwa kidonda kingine chochote kilichovimba.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mng'ato wa nyoka una sumu?

Ili kujua kama mng'ato wa nyoka una sumu, daktari wako ataangalia alama za mng'ato. Daktari atauliza nyoka alikuwa anakaa aje. Daktari pia atauliza kuhusu dalili zako.

Is That a Pit Viper?

Pit vipers have certain features that can help distinguish them from nonvenomous snakes:

  • Vertical slitlike pupils

  • Pits between the eyes and nose

  • Retractable fangs

  • Rows of single scales across the underside of the tail

  • Triangular heads (like an arrowhead)

Nonvenomous snakes tend to have the following:

  • Rounded heads

  • Round pupils

  • No pits

  • No fangs

  • Rows of double scales across the underside of the tail

If people see a snake with no fangs, they should not assume it is nonvenomous because the fangs may be retracted.

Umbo la mng'ato wakati mwingine linaweza kusaidia kujua kama nyoka huyo ni mwenye sumu:

  • Ming'ato ya nyoka wasio na sumu kwa sana huacha safu za mikwaruzo midogo

  • Ming'ato kutoka kwa nyoka wenye sumu kwa sana huwa pancha moja au mbili kubwa (mashimo)

Je, madaktari wanatibu vipi mng'ato wa nyoka?

Kwa mng'ato wa nyoka asiye na sumu, madaktari watautibu kama vile tu wanavyotibu majeraha ya kutobolewa. Atafanya yafuatayo:

  • Kusafisha kidonda

  • Kukupa dawa ili kuzuia maambukizi, kama inavyohitajika

  • Kuangalia kama ulipewa chanjo ya pepopunda katika miaka 5 iliyopita na akuchanje ikiwa haujapewa chanjo

Kwa mng'ato wa nyoka mwenye sumu, daktari:

  • Atakupatia kiuasumu ya nyoka (dawa ambayo hufanya kazi dhidi ya sumu mahususi) kupitia IV (kwenye mshipa wako)

  • Atakuweka hospitalini kwa hadi saa 6 hadi 8 ili kuangalia dalili zako, na muda zaidi ikiwa inahitajika

  • Atakuweka kwenye huduma ya wagonjwa mahututi kwenye hospitali, ikiwa ulipata kiwango cha juu cha sumu ya nyoka