Uonevu ni nini?

Uonevu ni kumdhuru mtu mwingine kwa vitendo (kama vile kumgonga mtu au kuvunja vitu vyake) au maneno (kumtania, kumchokoza, au kumtishia). Mchokozi anaweza kuwa mkubwa, mwenye nguvu, au mwenye umaarufu zaidi kuliko mwathiriwa.

Uonevu unaweza kutokea katika maeneo mengi, kama vile nyumbani, shuleni, au kazini. Unaweza kufanyika mara moja au ujirudie mara nyingi.

  • Wavulana na wasichana kwa pamoja wanaweza kuwa waonevu

  • Uonevu unaweza kufanyika katika umri wowote, kutoka umri wa kabla ya shule hati utu uzima

  • Wanafunzi wengi huonewa kupitia barua pepe, ujumbe mfupi, na mitandao ya kijamii (hali hii inaitwa unyanyasaji wa mtandaoni)

  • Kuonewa au kuonea watu si sehemu ya kawaida ya maisha ya utotoni

Kutuma ujumbe wa ngono ni utumaji wa kidijitali wa ujumbe au picha za ngono kwa mtu mwingine. Utumaji wa ujumbe wa ngono unaweza kusababisha uonevu ikiwa mtu anataka kumuumiza au kumwaibisha mtu ambaye picha au ujumbe wake wa ngono ulitumwa.

Ninawezaje kujua iwapo mtu anaonewa?

Watu wanaoonewa wanaweza:

  • Huzunika

  • Kuwa na fedheha

  • Kuwa na majeraha

  • Wasiwasi

  • Kutojiamini

Mwathiriwa wa uonevu mwenye umri mdogo anaweza kuona aibu kumwambia mtu mzima. Walimu na wazazi mara nyingi huwa hawagundui kuwa mtoto anaonewa. Waathiriwa wengi huathiriwa kimwili na/au kihisia kutokana na kuonewa.

Waonevu hujifunza tabia mbaya ambazo zisiporekebishwa, zinaweza kusababisha vurugu zaidi. Waonevu wana uwezekano mkubwa wa kushindwa kusalia shuleni, kuajiririwa, au kuwa na mahusiano thabiti wakiwa watu wazima, na wana uwezekano mkubwa wa kufungwa gerezani katika maisha yao ya baadaye.

Ninapaswa kufanya nini ikiwa ninaonewa?

Uonevu ni mbaya. Ikiwa mtu anakuonea, unapaswa:

  • Kumwambia mtu mzima

  • Kumwondokea

  • Kubadilisha shughuli zako za kila siku ili umwepuke anayekuonea

  • Kuzungumza na tabibu au mshauri wa kisaikolojia

  • Kujifanya kana kwamba unapuuza uonevu huo ili anayekuonea apoteze hamu ya kuendelea

Ikiwa uonevu unafanyika shuleni, wafahamishe viongozi wa shule.

Ninapaswa kufanya nini ikiwa mtu mwingine anaonewa?

Usipuuze uonaji huo. Kitu cha muhimu zaidi cha kufanya unapotambua kuwa mtu anaonewa ni kushughulikia hali hiyo mara moja.

Ikiwa mtoto wako anaonewa:

  • Waambie viongozi wa shule

  • Mkumbushe mtoto wako kuwa uonevu si mzuri

  • Mwambie mtoto wako ajaribu kumpuuza anayemwonea

  • Zungumza na wazazi wa mtoto anayemwonea (lakini usionyeshe hasira ila angazia tabia isiyofaa ya mtoto wao), na umwombe mwoneaji aombe msamaha na aache uonevu

  • Mtafutie mtoto wako usaidizi wa ushauri nasaha

Je, maelezo zaidi yanapatikana wapi?